Wakulima huko Mwanza Tanzania waomba kiwanda cha usindikaji nyanya

5 Septemba 2016

Jarida letu maalum leo Jumatatu ikiwa ni siku ya mapumziko nchini Marekani, linakupeleka Mwanza nchini Tanzania kuangazia harakati za wakulima na kilio chao cha nini kifanyike kuweza kuwakwamua. Hii inatokana na ukweli kuwa katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu,namba moja ikiwa ni kutokomeza umaskini, kilimo kinaonekana kuwa moja ya maeneo ambayo yanapaswa kupatiwa kipaumbele ili kunasua wakulima. Je nini kinafanyika? Martin Nyoni wa Radio washirika Radio SAUT FM kutoka Mwanza amevinjari kukutana na wakulima na wadau wa kilimo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter