Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wawajibikaji wa shambulio Davao waletwe mbele ya sheria-Ban

Wawajibikaji wa shambulio Davao waletwe mbele ya sheria-Ban

Katibu Mkuu Ban Ki-moon leo amelaani shambulio la bomu lililotokea Ijumaa, katika soko la usiku katika mji wa Davao, Ufilipino, lililokatili watu 12 na kujeruhi wengine.

Katika taarifa yake kwa kupitia msemaji wake, Ban amesisitiza haja ya kuhakikisha uwajibikaji na kuwaleta mbele ya sheria wahusika wa mashambulizi haya ya kigaidi.

Ban ametoa salamu zake za rambirambi kwa familia ya wahanga na kuwatakia majeruhi afueni haraka, na amesema Umoja wa Mataifa unasimama pamoja na serikali na watu wa Ufilipino.