Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumesikia mengi kutoka Sudan Kusini-Baraza la Usalama

Tumesikia mengi kutoka Sudan Kusini-Baraza la Usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama leo wamekutana na Baraza la Mawaziri , wawakilishi kutoka jumuiya ya asasi za kiraia, vikundi vya wanawake, vijana na mashirika ya kidini katika ziara yao ya siku tatu nchini Sudan Kusini.

Katika mkutano na mawaziri, wajumbe hao wamesitiza ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Sudan Kusini. Mmoja wa viongozi wa ziara hiyo, Balozi Samantha Power mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa amesema, mkutano na mawaziri ulikuwa mzuri, na pande zote mbili zilisikilizana na kukubaliana jinsi ya kusonga mbele katika kutimiza matakwa ya pande zote mbili.

Wajumbe hao pia wamekutana na wanawake, ambapo wamesikia kilio chao cha kuongezeka kwa ubakaji, pindi wanapoenda kusaka kuni kwa ajili ya kuwapikia watoto wao chakula ambapo Balozi Power amesema..

(Sauti ya Balozi Power)

“Nikiwa mama, naweza kufikiria ni jinsi gani unachagua; kuchagua kupikia watoto au nijiweke hatarini kwa kwenda nje ya kambi na kubakwa. Nafahamu nitakwenda na nitajiweka hatarini kwa ajili ya wanangu. Nafikiri mama yeyote atafanya hivyo.”

Baadaye wajumbe hao walizuru pia kituo cha ulinzi wa raia katika jengo la Ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNMISS kutathmini hali ilivyo.