Mazungumzo ya kitaifa yaanza DRC, Ban afuatilia

Mazungumzo ya kitaifa yaanza DRC, Ban afuatilia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepata taarifa za kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC tarehe Mosi mwezi huu na anafuatilia kwa karibu.

Taarifa ya msemaji wake imemnukuu akisema kuwa bado anaamini kuwa mjadala shirikishi wa kisiasa ndio njia pekee ya kuwezesha kufanyika uchaguzi halali na wa amani.

Hivyo amehimiza makundi mengine ya kisiasa ambayo hayajajiunga, kuingia katika mazungumzo hayo ili nayo yapate fursa ya kuchangia katika uchaguzi muafaka.

Amesihi wadau wote kufanya kila wawezalo kujizuia na tabia zozote zitakazoleta vurugu.

Pia ameisihi serikali kuendeleza hatua za kujenga imani na kuzingatia haki za msingi na uhuru kama ilivyo kwenye katiba.