Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Sri Lanka kiri sauti za walioathirika - Ban

Serikali ya Sri Lanka kiri sauti za walioathirika - Ban

Katibu Mkuu wa Umoja Ban Ki-moon ametoa wito kwa viongozi wa Sri Lanka kukubali sauti za waathirika kwa maovu yaliyotendeka hapo zamani.

Akizungumza na vijana kwenye mji mkuu Colombo, Bwana Ban amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanywa ili kuondoa makovu ya madhila yaliyopita na kurejesha uhalali na uwajibikaji wa taasisi muhimu nchini humo hasa mahakama na huduma za usalama.

Hata hivyo ameipongeza hatua ya serikali ya kurejesha tume ya haki za binadamu lakini amesema inapaswa kuheshimiwa, kuaminiwa na kupatiwa rasilimali.

Amesema kwa kufanay hivyo itaweza kushughulikia haki za binadamu kwa ufanisi, jambo ambalo amesema ni muhimu kwa maridhiano.

Amewahimiza wenye mamlaka kuharakisha kurejesha kwa ardhi ili watu waliokimbia makazi yao wanaweza kurejea makwao. Sri Lanka imekuwa na migogoro ya zaidi ya miaka 25 iliyofikia ukomo mwaka 2009 lakini tuhuma za manyanyaso kutoka kwa waasi na serikali zinaendelea.