Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waimbaji katika harakati za kurejesha sanaa ya muziki Cambodia

Waimbaji katika harakati za kurejesha sanaa ya muziki Cambodia

Muziki ni sanaa ambayo ilikaribia kutoweka wakati wa mauaji ya kimbari, yaliyofanyika katika kipindi cha mamlaka ya Khmer Rouge huko Cambodia,  sasa ipo njiani kurejeshwa. Hii imewezeshwa na  msaada wa shirika lisilo la kiserekali, ambalo kazi yake ni kushirikisha wasanii wa muziki wa asili na kizazi kipya ili kuendeleza na kuhifadhi utamaduni huu. Moja ya bendi inayoshiriki katika harakati hizi ni Dengeu Fever. Basi tuungane na Bryan Lehander kufahamu zaidi.