Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Kyrgystan.

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Kyrgystan.

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la bomu dhidi ya ubalozi wa China huko Kyrgyzstan.

Shambulio hilo la tarehe 30 Agosti kwenye mji mkuu, Bishkek, lilisababisha majeraha kwa wafanya kazi wa ubalozi huo.

Katika taarifa yao, wanachama hao wamewatakia ahueni ya haraka majeruhi sambamba na kwa familia zao na serikali za China na Kyrgyzstan.

Halikadhalika wanachama wa Baraza la Usalama wamesema wanatambua juhudi zinazoendelea nchini humo za serikali kuchunguza kikamilifu shambulio hilo la kigaidi  na kutaka wahusika, waandaaji na wahisani wafikishwe mbele ya sheria.

Na katika kutekeleza hilo wamesihi nchi zote kushirikiana kwa kuzingatia wajibu wao kwa mujibu wa sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama.