Skip to main content

Tangu kifo cha mtoto Alan, maafa bado yaongezeka- UNHCR

Tangu kifo cha mtoto Alan, maafa bado yaongezeka- UNHCR

Ni mwaka mmoja sasa tangu dunia  ishuhudie  picha  ya Alan Kurdi,  mtoto kutoka Syria ambaye alipatwa na mauti wakati boti alimokuwa akisafiria na familia yake kuzama bahari ya Mediteranea wakati  wakieleka Ulaya kusaka hifadhi.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, huko Geneva, Uswisi, William Spindler  amesema inakadiriwa  kuwa  tangu  kifo cha Alan,  kuna  zaidi ya watu  Elfu Nne waliopoteza maisha kwenye bahari ya mediterania, mwaka huu pekee.

Amesema mwaka huu umekuwa wa maafa zaidi katika historia kwenye bahari hiyo akisema…

(Sauti ya Willliam)

 Nafasi ya kupatwa na mauti kutoka Libya kwenda Italia ni mara kumi zaidi ukilinganisha ile ya kuvuka kupitia Uturuki kwenda Ugiriki. Kutokana na maafa haya ya kila kukicha, kuna umuhimu wa nchi husika kufikia mbinu mbadala ikiwa pamoja na hifadhi ya kudumu kwa wakimbizi, wahisani binafsi wajitokeza na pia kunganisha familia zilizotengwa ili kupunguza maafa katika safari hizi hatari baharini.