Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Beyani kumulika haki za wakimbizi wa ndani Ukraine

Beyani kumulika haki za wakimbizi wa ndani Ukraine

Mwakililishi Maalum wa umoja wa mataifa wa haki za kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani leo ameanza ziara ya siku saba nchini Ukraine.

Ziara yake ni ya kufuatilia jinsi hali ya wakimbizi wa ndani ilivyo nchini humo na pia kufuatilia mapendekezo aliyotoa katika ripoti yake kwa baraza la haki za kibinadamu la Umoja wa mataifa.

Amesema ataangalia hatua zilizochukuliwa katika kulinda na kutoa usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na pia kushauriana kuhusu changamoto na nafasi walizo nazo za kujiendeleza wenyewe nchini Ukraine.

Akirejelea ziara yake ya kwanza, Bwana Beyani amesema kuwa amekuwa akifuatilia kwa karibu hali ilivyo kwa wakimbizi wa ndani nchini Ukraine na bado wanapata changamoto katika kupata haki zao, huduma za kijamii za umma na hata uhuru wa kusafiri na ajira.

Wakati wa ziara yake Beyani atakutana na viongozi wa serikali, washirika wa Umoja wa Matafa, vyama vya kiraia na wakimbizi wa ndani na jamii husika.