Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa ndani wapata makazi mapya huko Najaf, Iraq – UNHCR

Wakimbizi wa ndani wapata makazi mapya huko Najaf, Iraq – UNHCR

Makazi mapya kwa wakimbizi wa ndani nchini Iraq leo yalifunguliwa rasmi katika mji wa Najaf nchini humo, shughuli ambayo ilishuhudiwa na mwakilishi wa shirika la kuhudumia wakimbizi, la Umoja wa Mataifa, UNHCR, nchini Iraq Bruno Geddo.

Makazi hayo yapatayo 100 yamejengwa katika kambi ya Al Najaf, yakijumuisha huduma za usafi wa mazingira na vifaa vya jikoni kwa wakazi wake.

Taarifa ya UNHCR inasema idadi kubwa ya wanufaika wamehamia eneo hilo baada ya kufukuzwa kutoka maeneo mengine.

Mwakilishi huyo wa UNHCR aliishukuru mamlaka ya Najaf kwa mshikamano wao wakuhami jamii hizo baada ya kukimbia makwao kutokan na migogoro.

Zaidi ya familia 14,600 zilizopoteza makazi zikiwa ni jumla ya watu 87,800 wanaishi Najaf.