Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya manjano Angola na DRC si tishio kwa afya ya umma duniani- WHO

Homa ya manjano Angola na DRC si tishio kwa afya ya umma duniani- WHO

Shirika la afya duniani, WHO limesema mlipuko wa homa ya manjano huko Angola na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC haujasababisha udharura wa afya ya umma kimataifa.

Kamati ya dharura ya WHO iliyokutana Geneva, Uswisi imesema hata hivyo hatua zaidi zinahitajika kukabili ugonjwa huo unaoendelea kuenea katika nchi hizo.

Oyewale Tomori, ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo kuhusu homa ya manjano amesema chanjo ndiyo msingi wa kukabili ugonjwa huo ambapo tayari dozi milioni 28 zimetolewa kutoka bohari ya kimataifa ya dharura tangu mwezi Februari mwaka huu.

Hata hivyo amesema kutokana na uhaba wa chanjo, wanachofanya ni kuizimua kidogo ili kuongeza idadi ya wanaopata chanjo huko Angola na DRC na kwamba kinga inakuwa ni kwa mwaka mmoja.

(Sauti ya Tomori)

“Tumesikia kuwa Kinshasa wamekamilisha kampeni ya matarajio makubwa zaidi kuwahi kufanyika. Ndani ya siku 10, zaidi ya watu Milionis aba nukta saba mjini Kinshasa walipatiwa chanjo, na wengi wao kwa chanjo mpya dhidi ya homa ya manjano ambayo imezimuliwa.”