Utamaduni wa amani wajadiliwa New York

1 Septemba 2016

Leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu kuhusu utamaduni wa amani ambapo Rais wa baraza hilo Mogens Lykettoft amesema ukuzaji wa utamaduni wa amani ni muhimu zaidi katika dunia ya leo iliyoghubikwa na mizozo. Taarifa kamili na Brian Lehander.

(Taarifa ya Brian...)

Nats..

Tumbuizo hii ya muziki katika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu amani…kuandaa fikra za washiriki..

Mwenyeji wa mkutano huu, Mogens Lyketoft katika hotuba yake amesema mizozo katika pande zote za dunia, iwe mapigano makubwa ya Syria, Yemen na Sudan Kusini, au ugaidi wa ISIS, ama mapigano baina ya jamii yamesababisha vifo na majeraha kwa maelfu ya mamia ya watu na kusambaratisha mamilioni wengine, hivyo..

(Sauti ya Mogens)

"Wakati Umoja wa Mataifa unasherehekea miaka 70 tangu kuanzishwa kwake, kuboresha uwezo wake wa kuendesha shughuli za amani na kudumisha amani sio msingi wa kutuliza migogoro, bali ni muhimu katika kufikia malengo 17 ya maendeleo endelevu yaliyopitishwa miezi 12 iliyopita"

Naye mwakilishi wa Katibu Mkuu Edmund Mulet amesema ni lazima vijana kushiriki kikamilifu wakati wa mijadala ya amani kwani ndio kizazi kijacho

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter