Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti wapendekeza kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania

Utafiti wapendekeza kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania

Utafiti uliofanywa nchini Tanzania kwa ushirikiano kati ya shirika la kazi duniani ILO na serikali kuhusu hifadhi ya jamii umependekeza kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii ili iweze kutoa huduma bora zaidi kuliko hivi sasa.

Akihojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo, mratibu wa taifa wa hifadhi ya jamii ILO Dampu Nicholous Ndenzako amesema utafiti huo ulizingatia kuwa kila mfuko ulianzishwa kwa ajili ya kuhudumia sekta fulani na kuripoti katika mamlaka tofauti kwa hiyo..

(Sauti ya Dampu)

Miongoni mwa sekta zenye changamoto katika kujiunga na hifadhi ya jamii ni walinzi kutoka kampuni binafsi ambapo Hawa Wenga afisa kutoka ofisi ya waziri mkuu nchini humo amesema..

(Sauti ya Hawa)