Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atiwa wasiwasi na mvutano huko Sahara Magharibi

Ban atiwa wasiwasi na mvutano huko Sahara Magharibi

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza wasiwasi wake juu ya mvutano unaoendelea huko Sahara Magharibi kwenye eneo ambalo lililokuwa chini ya Hispani hadi mwaka 1976 ambapo mapigano yalizuka katika Morocco na kikundi cha Polisario.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa Jumapili imesema wasiwasi huo unatokana na mvutano kwenye ukanda wa eneo la hifadhi huko kusini-magharibi mwa Sahara Magharibi, katikati ya Morocco na Mauritania

Ban amesema hali hiyo ya mvutano inatokana na mabadiliko  yaliyotokea na kuwekwa kwa vikundi vyneye silaha kutoka Morocco karibu na vile vya Polisario.

Ban ametaka pande zote kusitisha vitendo vyao ambavyo vinaweza kubadilisha hali ilivyokuwa awali na kwamba vikosi hivyo viondolewe ili kuepusha mvutano zaidi.

Amesema kwa kufanya hivyo, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINURSO utaweza kuwa na mazungumzo na pande zote huku akizikumbusha pande hizo ziwajibike kwa kuzingatia makubaliano yam waka 1996 ya kusitisha mapigano.