Skip to main content

Kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya polio kufanyika Afghanistan

Kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya polio kufanyika Afghanistan

Nchini Afghanistan, kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya polio imeanza leo kwa watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano, kwa kuwa ugonjwa huo hulipuka kati ya mwezi Septemba na Oktoba.

Shirika la afya duniani, WHO limesema kampeni hiyo inayofanywa kwa ushirikiano baina yake, wizara ya afya ya umma nchini humo na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF inatekelezwa na wafanyakazi wa afya wapatao 65,000.

Wahudumu hao wenye mafunzo watakwenda hadi maeneo ya kuvuka mpaka na Pakistani ambako kuna wakimbizi zaidi ya milioni moja na nusu wa Afghanistani.

Kampeni hiyo ilianza jumatatu na siku ya Ijumaa kutafanyika ufuatiliaji kuona iwapo kuna mtoto yoyote aliyekosa chanjo dhidi ya polio, ugonjwa ambao husababisha ulemavu kwa watoto.