Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kushuka kwa bei ya mafuta na athari zake Afrika

Kushuka kwa bei ya mafuta na athari zake Afrika

Kushuka kwa bei ya mafuta katika miaka miwili iliyopita kumetikisa uchumi wa nchi nane Afrika, amesema Abebe Selassie, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya shirika la fedha duniani, IMF. RoseMary Musumba na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Rose).

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa ametaja nchi athirika zaidi kuwa ni pamoja na Angola , Equatorial Guinea na  Nigeria ambazo zimeshuhudia kushuka kwa bei ya mafuta kutoka dola 125 kwa pipa hadi dola 50. Athari ni pamoja na kupungua kwa kasi ya mapato ya kuuza bidhaa nje na nakisi ya fedha.

Hata hivyo kushuka kwa bei ya mafuta kumekuwa na faida kwa nchi ambazo zinatarajia kuzalisha mafuta kama Tanzania na Msumbiji..

(Sauti ya Abebe)

"Nchi hizi hazijaanza kuzalisha mafuta bado, kwa hiyo hawataathiriki na kushuka kwa bei, swali muhimu la kuuliza  ni je kuna manufaa  katika kuwekeza na kuendeleza miradi hii, na maoni ni kwamba kama umepata kitu chenye thamani kubwa ndani ya ardhi, matarajio ya athari yake, sio sababu ya kuiacha  ardhini"

Aidha ametoa wito kwa watunga sera katika nchi hizo kuzingantia uchumi mseto kama uzalishaji wa nishati,  ukuzaji wa sekta ya kilimo ili kuepuka na kutegemea mapato ya mafuta pekee.