Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Keating alaani shambulio Mogadishu

Keating alaani shambulio Mogadishu

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Michael keating, amelaani vikali shambulizi la bomu kwenye hoteli ya SYL mjini Mogadishu.

Watu 13 waliuawa na wengine 20 walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo lililotokea wakati maafisa waandamizi wa serikali na wabunge walipokuwa wanashiriki mkutano ndani ya hoteli hiyo.

Taarifa ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Somalia, UNSOM ambayo Keating ndiyo kiongozi wake, imesema hakuna kiongozi yoyote miongoni mwao aliuawa au kujeruhiwa katika tukio hilo ambalo Al Shabaab wamekiri kuhusika.

Keating amesema hii ni mara ya tatu tangu mwaka 2015 hoteli hiyo inashambuliwa na magaidi lakini ni kiashiria vile ambavyo wananchi wa Somalia hawakubali kujisalimisha na kuwa waoga dhidi ya magaidi.