Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan tupilieni mbali mashtaka dhidi ya watetezi wa haki- Wataalamu

Sudan tupilieni mbali mashtaka dhidi ya watetezi wa haki- Wataalamu

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wametaka mamlaka za Sudan kutupilia mbali mashtaka dhidi ya watu sita wanaohusika na shirika moja lisilo la kiserikali nchini humo, TRACKS. Taarifa kamili na Brian Lehander.

(Taarifa ya Brian)

Mashtaka hayo ikiwemo kukandamiza mfumo wa kikatiba, uhaini na ugaidi, adhabu yake ni kifo ambapo wataalamu hao wamesema adhabu hiyo ni kupindukia na iwapo inapaswa kutumika ni lazima izingatia mchakato wa kina unaozingatia sheria za kimataifa.

Aristide Nononsi ambaye ni mtaalamu huru wa haki za binadamu kwa Sudan amesema watu hao sita wakiwemo wanawake wawili walikamatwa miezi mitatu iliyopita lakini hadi sasa hawajafikishwa mahakamani ambapo mashtaka dhidi yao yanaonekana ni kutokana na kazi yao ya utetezi wa haki za binadamu.

Nononsi amesema kundi lao linataka serikali ya Sudan iruhusu watetezi hao kufanya kazi katika mazingira huru kwani wana dhima kubwa katika mustakhbali wa nchi.