De Mistura ahuzunishwa na kuendelea kwa mapigano Syria

De Mistura ahuzunishwa na kuendelea kwa mapigano Syria

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura amesema anasikitishwa mno na kuendelea kwa mapigano na hali ya hatari ya kibinadamu nchini humo.

Katika taarifa yake, amesema mchakato wa kisiasa na suluhu la kisiasa ndio njia pekee ya kumaliza mgogoro huo na hali ilivyo kwa sasa.

Ameongezea kuwa majadiliano kati ya Urusi na Marekani wiki hii ni muhimu kwa jitihada za kurejesha ukomeshaji wa uhasama.

Bwana de Misturra amesema Umoja wa Mataifa nao pia unaendelea na mashauriano yake na wenye viti wa kamati ya kimataifa ya usaidizi kwa Syria, ISSG na wanachama wake ili kuleta suluhisho.

Kuhusu ombi la sitisho la mapigano kwa maslahi ya kibinadamu huko Aleppo kwa saa 48, de Misturra amesema hoja hiyo bado ipo na hakuna pande yoyote iliyoitupilia mbali.