Skip to main content

Mamilioni ya wanafunzi Afika ya Kati na Magharibi hatarini kukosa chakula

Mamilioni ya wanafunzi Afika ya Kati na Magharibi hatarini kukosa chakula

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limeonya kuwa zaidi ya watoto Milioni Moja nukta tatu mamilioni huko Afrika  ya kati na magharibi wako hatarini kukosa mlo wa shuleni wakati  huu ambapo shule zinakaribiwa kufunguliwa mwezi ujao.

WFP inasema hali hiyo inatokana na upungufu wa bajeti kutoka kwa wahisani kwa kuwa wahisani wamepatia kipaumbele nchi zenye uhitaji zaidi katika masuala ya kijamii.

Bettina Luescher msemaji wa WFP, Geneva anasema hali hii inatia hofu kubwa kwa sababu…

(Sauti ya Bettina)

“Watoto laki tano huko watoto huko Cameroon, Mali, Mauritania na Niger wanaweza kuanza mwaka wa shule bila mlo ambao umekuwa ni tegemeo lao. Hili ni jambo muhimu kwa sababu kwa familia nyingi wamekuwa wanafahamu kuwa mlo kamili unatolewa na WFP.”