Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saa 48 zashuhudia kuokolewa zaidi ya watu 7,000 huko Mediteranea

Saa 48 zashuhudia kuokolewa zaidi ya watu 7,000 huko Mediteranea

Zaidi ya watu elfu saba waliokolewa kutoka bahari ya Mediteranea juzi jumapili na jana jumatatu karibu na pwani ya Libya.

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limesema idadi kubwa ya watu hao walikuwa wakisafiri kwa boti zisizo salama ikiwemo zile za kujazwa upepo, za mbao na nyingine za uvuvi.

Joel Millman ni msemaji wa IOM.

 “Tuna taarifa za watu wawili kupoteza maisha jana, tumeona picha. Watu wengi walikuwa na majaketi ya uokozi jambo ambalo ni jema. Lakini idadi inaweza kuwa kubwa, lakini hadi sasa tuna ripoti za vifo viwili.”

Kwa mujibu wa IOM zaidi ya watu Laki Moja wameokolewa kutoka karibu na pwani ya Libya mwaka huu pekee.