Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kuboresha takwimu za sekta za nje waanzishwa na Shirika la Fedha Duniani

Mradi wa kuboresha takwimu za sekta za nje waanzishwa na Shirika la Fedha Duniani

Shirika la fedha duniani, IMF, hii leo limezindua mradi wa miaka mitatu wa kuboresha takwimu za sekta katika nchi za Afrika ya Kati na a Magharibi.

Mradi huo umeanzishwa katika taasisi ya mafunzo ya Afrika, ATI, huko nchini Mauritius na umewezeshwa kwa msaada mkubwa wa serikali ya Japan.

Mradi huo una lengo la kuimarisha takwimu za sekta za nje, kuleta ubora na kufunga mapengo katika maeneo muhimu kama vile urari wa malipo, nafasi ya kimataifa ya uwekezaji na takwimu za nje za madeni.

Bwana Louis Marc Ducharme, ambaye ni mkurugenzi wa idara ya takwimu huko IMF, aliipongeza hatua hiyo akisema itawapatia washiriki fursa ya kujadili changamoto za pamoja, kubadilishana maoni na kujihamasisha kwa nia ya kuboresha takwimu zao za sekta ya nje.

Washiriki wa warsha ya uzinduzi wa mradi huo walikuwa maofisa wa benki wa ngazi za juu na kati kutoka nchi 17 zinazozungumza kifaransa na wawakilishi wa Benki kuu ya Mataifa ya Afrika Magharibi, (BCEAO) and Benki Kuu ya mataifa ya Afrika ya kati (BEAC).