Vifaa vya matibabu vyawasili Taiz, Yemen

Vifaa vya matibabu vyawasili Taiz, Yemen

Shirika la afya duniani WHO na msaada wa kituo cha misaada ya kibinadamu cha mfalme Salman limetoa msaada wa tani kumi na mbili za vifaa vya matibabu ya dharura kwa jiji la Taiz nchini Yemen.

Taarifa ya WHO imesema vifaa hivyo ni pamoja na dawa za kutibu kipindupindu na vifaa vya kusaidia watoto wanaozaliwa, unatarajiwa kusambazwa kwa wakazi wa jiji hilo pamoja na hospitali za Al- Thawra, Al-Modhaffar na Al- Ta'aon ambako wamekumbwa na ghasia za kivita

Mwakilishi wa WHO nchini Yemen, Dkt. Ahmed Shadoul amesema kufikishwa kwa misaada hiyo ni hatua kubwa kwa sababu huduma za kiafya jijini Taiz zimezorota baada ya kukumbwa na ukosefu mkubwa wa vifaa.