Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC yaongelea kukuza usalama na maendeleo Afrika

UNODC yaongelea kukuza usalama na maendeleo Afrika

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC, Bwana, Yury Fedotov amesema ataendelea kushirikiana na serikali ya Kenya na nchi jirani kuimarisha uwezo wa kupambana na uhalifu kama vile ugaidi, rushwa, madawa ya kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu.

Bwana Fedotov amesema hayo alipokutana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kando mwa mkutano wa Sita wa kimataifa wa Tokyo kwa maendeleo ya Afrika, TICAD uliofanyika Nairobi .

Amemshukuru Rais Kenyatta kwa ushirikiano wa muda mrefu kati ya kenya na  UNODC, ikiwa ni pamoja na jitihada za kukuza maendeleo, usalama na haki kwa nchi za Afrika mashariki.

Bwana Fedetov pia alikutana na viongozi toka nchi mbalimbali za Afrika ambao ni wanachama wa mkutano huo wa TICAD.