Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tofauti za kihistoria zisikwamishe maendeleo ya Asia- Ban

Tofauti za kihistoria zisikwamishe maendeleo ya Asia- Ban

Akiwa ziarani barani Asia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema itakuwa jambo la kusikitisha iwapo bara hilo litaendelea kukwamisha na tofauti zao za kihistoria badala ya kusonga mbele kimaendeleo.

Akitoa mhadhara kwenye chuo kikuu cha uongozi huko Singapore, Ban ametaja masuala hayo ya kihistoria kuwa ni migogoro ya mipaka, na mkanganyiko katika tafsiri ya historia.

Amesema bara hilo linatakiwa liwe na mtazamo wa baadaye wa mustakhbali wa pamoja utakaoweza kumaliza mikanganyiko hiyo na suluhu za mizozo kadhaa ikiwemo suala la nyuklia katika rasi ya Korea.

Ziara ya Ban huko Asia itampeleka pia Myanmar, Sri Lanka, Laos na China ambako atashiriki mkutano wa viongozi wa kundi la nchi 20, G-20.