Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD na WFP zatia saini mkataba wa kuendeleza kilimo Sudan

IFAD na WFP zatia saini mkataba wa kuendeleza kilimo Sudan

Shirika la kimataifa la ufadhili wa maendeleo ya kilimo, IFAD na lile la mpango wa chaukula duniani, WFP, hii leo wametia saini makubaliano ya kuendeleza uhakika wa chakula kwa kuendeleza kilimo miongoni mwa wakulima wadogo wadogo nchini Sudan. RoseMary Musumba na taarifa kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

Kupitia makubaliano hayo mashirika hayo mawili yatakuwa na jukumu la kuongeza ubora na upatikanaji wa rasilimali za kilimo kwa wakulima hao.

Hii ni pamoja na kuwapatia mbegu bora, mafunzo kuhusu mikopo ya kilimo na mbinu za kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno.

Ikiwa pia na kazi ya kuboresha upatikanaji wa huduma za soko kwa mazao,  makubaliano hayo yatazingatia pia sera na ufuatiliaji wa athari ya hali ya hewa katika kilimo, lengo lake likiwa ni kusaidia jamii kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mwakilishi mkazi wa WFP huko Sudan Adnan Khan amesema makubaliano hayo ni mfano bora wa kupanua ushirikiano kati ya mashirika hayo mawili.