Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa usawa wa kijinsia wagharimu Afrika mabilioni ya dola- Ripoti

Ukosefu wa usawa wa kijinsia wagharimu Afrika mabilioni ya dola- Ripoti

Ripoti mpya kuhusu maendeleo ya binadamu barani Afrika imesema ndoa katika umri mdogo zimeendelea kuwa kikwazo katika maendeleo ya kijinsia barani humo.

Kwa mujibu wa Ayodele Odusola, mchumi mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP lililoandaa ripoti hiyo iliyozinduliwa leo huko Nairobi, Kenya, watoto wa kike wanakwamia elimu ya msingi baada ya kupatiwa ujauzito, hivyo amesema..

(Sauti ya Ayodele)

Ripoti pia imependekeza kuanzishwa kwa benki ya uwekezaji ya wanawake barani Afrika ambapo mchumi huyo mkuu wa UNDP amesema…

(Sauti ya Ayodele)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Ukosefu wa usawa wa kijinsia kwenye soko la ajira kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, umegharimu zaidi ya dola Bilioni 90 kila mwaka kati ya mwaka 2010 na 2014.