Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sakata la vazi la Burkini, UN-Women yazungumza

Sakata la vazi la Burkini, UN-Women yazungumza

Wanawake wana haki ya kuchagua kuvaa kile watakacho bila shinikizo kutoka kwa serikali au mtu, amesema mkurugenzi wa sera katika shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN-Women, Purna Sen.

Bi. Sen amesema hayo akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa baada ya mahakama nchini Ufaransa kutupilia mbali katazo la mji moja nchini humo kuwa wanawake wasivae vazi la Burkini wanapokuwa ufukweni, vazi ambalo linavalia na wanawake wakiwemo waumini wa dini ya kiislamu.

Mahakama hiyo ilifuta katazo hilo leo baada ya picha kuonyesha jinsi polisi mmoja alivyokuwa anamshinikiza mwanamke mmoja atoe vazi hilo.

(Sauti ya Sen)

“Burkini bila shaka ni moja ya vazi ambalo limechaguliwa na baadhi ya wanawake na fursa yao ya kuvaa vazi hilo inapaswa kulindwa.”