Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupungua kwa visa vya Malaria, Kagera nchini Tanzania

Kupungua kwa visa vya Malaria, Kagera nchini Tanzania

Malaria! Ugojwa ulitambuliwa kuwa ugonjwa unaoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto barani Afrika. Hadi hivi karibuni ilitambuliwa kuwa kila dakika mtoto mmoja alikuwa anafariki dunia kutokana na Malaria barani humo ambako kati ya vifo 10 vya malaria, Tisa hutokea.

Lakini sasa kuna habari njema. Shirika la afya duniani, WHO linasema kuwa mambo yamekuwa mazuri na ugonjwa huo haungozi tena kwa kusababisha vifo vya watoto. WHO inataja mikakati iliyotumiwa kuwa ni matumizi ya vyandarua vyenye dawa, kupulizia dawa ndani ya nyumba ili kufukuza mbu na tatu kudhibiti visa vipya vya Malaria kwani huduma za uchunguzi na tiba zimesogezwa karibu na jamii. Katika kuthibitisha hilo tunakwenda Tanzania hususan mkoani Kagera ambako Nicolaus Ngaiza wa radio washirika Kasibante FM amevinjari kutathmini hali ya Malaria.