Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Colombia yajadiliwa barazani hii leo

Colombia yajadiliwa barazani hii leo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao cha faragha kuhusu Colombia ambapo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa umoja huo nchini humo  Jean Arnault amewasilisha taarifa kuhusu shughuli zilizofanyika tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo mwezi Januari mwaka huu.

Baada ya kikao hicho Malaysia ambayo inashikilia urais wa baraza hilo kwa mwezi huu wa Agosti ilitoa taarifa ya yale ambayo wajumbe wa baraza hilo wameafikiana kufuatia kuwasilishwa kwa ripoti hiyo ikiwemo makubaliano kati ya serikali ya Colombia na waasi wa FARC-EP ya kumaliza uhasama kati yao wa zaidi ya miaka 50.

Siti Hajjar Adnin ambaye ni naibu mwakilishi wa kudumu wa Malaysia kwenye Umoja wa Mataifa amesema wajumbe wa baraza wamekaribisha hatua hiyo iliyofikiwa huko Havana, Cuba

(Sauti ya Siti)

“Baraza limesisitiza azma yake ya kusaidia utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano, kusitisha kumaliza chuki, na kuweka chini silaha kwa usaidizi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa Colombia na kueleza kuunga mkono jitihada za mwakilishi a katibu Mkuu Jean  Arnault.