Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSOM yanoa wanahabari kuelekea uchaguzi nchini Somalia

UNSOM yanoa wanahabari kuelekea uchaguzi nchini Somalia

Warsha ya siku mbili ya kuwafundisha waandishi wa habari jinsi ya kuripoti habari za uchaguzi mkuu unaotarajiwa Somalia, imemalizika huku washiriki wakisema kuwa sasa wanajihisi tayari kuripoti vyema uchaguzi mkuu.

Washiriki walitoa shukrani kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM kwa kuandaa warsha hiyo iliyogusia mada kama vile uhuru wa wanahabari,sheria zinazoongoza uchaguzi na jukumu la Umoja wa mataifa katika uchaguzi huo.

Miongoni mwao ni Hsukri Ismael Ahmed Mtangazaji wa radio SWS ambaye amesema wamejifunza mengi katika warsha hiyo ikiwemo kutangaza habari bila upendeleo,jinsi ya kuripoti habari za uchaguzi, uhamasishaji wa wanawake kulingana na asilimia thelathini bungeni iliyotengwa rasmi kwa wanawake na mengine meng.

Naye mtangazaji wa radio ya Warsan Adan Hassan Osman amesema wameelezwa changamoto zile mwanahabari anaweza kukumbwa nazo wakati wa uchaguzi na jinsi anavyoweza kuzitatua.