Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gabon fanyeni uchaguzi kwa amani- Ban

Gabon fanyeni uchaguzi kwa amani- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa wananchi wa Gabon kushiriki katika uchaguzi mkuu hapo kesho kwa amani na kwa njia yenye kuaminika .

Ban pia ameipongeza serikali ya Gabon na Kamisheni ya Uchaguzi, CENAP kwa maandalizi muafaka na amekaribisha upelekwaji wa waangalizi wa uchaguzi wa kikanda na kimataifa, na kusisitiza umuhimu wake katika uchaguzi ulio wa wazi.

Stéphane Dujarric ni msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

(Sauti ya Stéphane )

"Katibu Mkuu anataka wadau wote wa kisiasa , hasa wagombea, kujizuia na vitendo vyovyote vya uchochezi au matumizi ya kauli za kichochezi, na badala yake wadumishe mazingira ya amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Anatoa wito kwa wagombea wote kuchangia katika uadilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kushughulikia kisheria na kikatiba malalamiko yoyote yatakayotokea".