Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani shambulio Kabul

Baraza la Usalama lalaani shambulio Kabul

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameshtumu vikali shambulizi la kikatili  huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistani.

Shambulizi hilo la Agosti 24 lililenga wanafunzi wa chuo kikuu cha kimarekani nchini ambapo watu wapatao 13 wakiwemo wanafunzi waliuawa na wengine 50 walijeruhiwa.

Katika taarifa yao, wanachama hao wametuma salamu za rambi rambi kwa jamii za waliofariki dunia na kwa watu na serikali ya Afghanistani.

Halikadhalika Baraza la Usalama limeleelezea wasiwasi wake juu ya vitisho vinavyotokana na vikundi vya Taliban, ISIL au Da’esh na makundi mengine ya haramu kwa wananchi, vikosi vya kijeshi na usalama nchini na vikundi vya kimataifa.