Kasi ya kuhamisha wahamiaji Ulaya inasuasua- UNHCR

Kasi ya kuhamisha wahamiaji Ulaya inasuasua- UNHCR

Wasaka hifadhi 160 wamewasili Ufaransa wakitokea Ugiriki chini ya mpango wa muungano wa Ulaya wa kuhamisha wahamiaji.

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limewezesha utekelezaji wa mpango huo uliojumuisha raia wa 128 wa Syria, 30 wa Iraq na wawili wasio na utaifa wowote.

Hata hivyo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema utekelezaji wa makubaliano kati ya muungano wa Ulaya na Uturuki kuhusu uhamishaji wasaka hifadhi unasuasua kwani idadi ya wanaohamishwa ni ndogo.

William Spindler, msemaji wa UNHCR, Geneva anaeleza kuwa nchi 24 za muungano wa Ulaya ziliahidi kupatia makazi mapya watu zaidi ya 160,000 lakini hadi sasa nafasi zilizopatikana ni zaidi ya12,000 na idadi halisi ya waliohamishwa ni chini ya Elfu Nne, hivyo amesema..

(Sauti ya William)

“Idadi ya watu walioahimishwa ni ndogo. Tunaona kwamba ahadi iliyotolewa na EU haitekelezwi na hii inatia wasiwasi kwa sababu hapa tuna mipango ya kushughulikia hali hii. “