Watoto wakimbizi Ugiriki mashakani- UNICEF

26 Agosti 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema idadi ya wakimbizi wanaoingia Ugiriki imeongezeka nchini Ugiriki kwa mwezi huu wa Agosti, huku hali ya watoto wakimbizi ikiwa ni ya kusikitisha. RoseMary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya RoseMary)

UNICEF inasema hali hiyo imetokea wakati kulikuwepo na fikra kuwa penginepo zahma inayokumba wakimbizi imepungua lakini Sarah Crowe, msemaji wa shirika hilo ambaye amerejea kutoka Ugiriki hivi karibuni amesema alichoshuhudia kinasikitisha..

(Sauti ya Sarah)

“Familia moja niliyokutana nayo, imetenga na baba yao  wakiwa njiani na mtoto huyo alifanya safari hiyo akiwa anaugua ugonjwa wa saratani. Na sasa anahaha kuungana na familia yake kwenda Ujerumani. Kuna simulizi nyingi za aina hii.”

Na kama hiyo haitoshi..

(Sauti ya Sarah)

“Kuna hisia kwamba watoto wanakumbwa na majanga mawili kwa sababu wamekwama Ugiriki, hawana uwezo wa kuendelea na maisha yao, na sasa mahitaji yanaongeza..elimu, afya na kadhalika.”

Amesema kwa sasa UNICEF wanajitahidi kuweka maeneo ya kuwawezesha watoto hao kujifunza ili angalau wawe na mwelekeo wa maisha.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter