Ban azungumza na Rais wa Italia Sergio Mattarella

25 Agosti 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, leo Alhamisi amezungumza na Rais wa Italia Bwana. Sergio Mattarella. Katibu Mkuu ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais huyo na watu wote wa Italia kufuatia vifo na uharibifu mkubwa uliosababishwa na tetemeko la ardhi la asubuhi ya Agost 24 ambapo mamia ya watu wamepoteza maisha.

Pia amepongeza juhudi kubwa na za haraka za uokozi zinazofanywa na serikali ya Italia , kuwanusuru na kuwasaidia walioathirika na tetemeko hilo.

Ban amemuhakikishia Rais wa Italia kwamba Umoja wa Mataifa unashikamana na serikali na watu wa Italia hasa katika kipindi hiki kigumu , lakini na siku zote.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter