Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza serikali ya Colombia na kundi la FARC-EP kwa muafaka

Ban apongeza serikali ya Colombia na kundi la FARC-EP kwa muafaka

Miaka Minne iliopita serikali ya Colombia na kikundi cha waasi FARC-EP walifikia muafaka wa kumaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda mrefu. Hatimaye hitimisho la mazungumzo ya kutafuta amani limefiakia ukingoni na wanatarajia  kuwatangazia  wananchi matokeo ya mstakabali wa taifa lao.

Katiku Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban-ki- moon kwa furaha kubwa amempogeza raisi wa Colombia Bw. Juan Manuel Santos, kiongozi wa upinzani Timoleon Jimenez na timu nzima ya washauri kutoka Havana kwa jitihada zao za kuhakikisha mazungumzo ya kutafuta amani nchini Colombia yanazaa matunda.

Pia amewashukuru wadhamini wa  mchakato wa kutafuta suluhisho, Cuba, Norway, Venezuela na chile, ikiwemo wananchi wa Colombia kwa kuruhusu  hali ya amani wakati viongozi wao wakiwa katika hali ya kutafuta suluhu ya matatizo yao.

Ban amesema kwa sababu muafaka wa amani umepatikana Colombia, sasa anayaomba mashirika ya kimataifa kuunga mkono Colombia katika hatua iliofikia kuleta amani chini mwao.

akiongeza kuwa Umoja wa mataifa siku zote utaendelea kuisaidia bega kwa bega serikali la Columbia katika jitihada za kutafuta amani pia kusaidia ujenzi mpya wa taifa hilo,