Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timu ya wakimbizi yarejea na kupokewa kwa shangwe

Timu ya wakimbizi yarejea na kupokewa kwa shangwe

Timu ya wakimbizi iliyoshiriki  kwa mara ya kwanza  michuano ya Olimpiki iliyomalizika mjini Rio De Janeiro nchini Brazil, imewasili na kupokelewa kwa nderemo mjini Nairobi Kenya hapo jana. Amina ana taarifa kamili.

( TAARIFA YA AMINA)

Nats!

Ngoma na bashasha zilitawala uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, pale mashujaa hao walipowasili na kupokewa kifalme. Hizi ni ngoma za utamaduni wa Burundi zilizoanikiza ujio huu.

Rose Lokonyen mwanariadha ambaye pai alipata heshima ya kubebea bendera ya Olimpiki akajivunia.

( SAUTI ROSE) (DADA ROSE)

‘Najisikia furaha sana  nilimaliza  mbio na pia nimepunguza muda ambao huwa nakimbia, nimapiga hatua na ninafuraha sana.’’

Licha ya kutopata medali, wakimbizi hao walimaliza katika mashindano kadhaa ikiwamo judo, kuogelea na kukimbia.

Yiech Biel naye alifukuza upepo.

( SAUTI YIECH) (BRIAN)

‘‘Hatukuwahi kutarajia kuwa tunaweza kwenda kweney Olimpiki. Lakini sasa dunia inafahamu wakimbizi. Ni sisi wakimbzi ndio tunaweza kufanya kazi kubadili dhana hiyo, kwakuwa nafahamu kuitwa mkimbizi ni jina tu. Unaweza kubadilisha .