Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia iko katika mwelekeo mzuri wa maendeleo: UNDP

Somalia iko katika mwelekeo mzuri wa maendeleo: UNDP

Mkurugenzi Mkuuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo UNDP Helen Clerk amesema licha ya machafuko, Somalia iko katika mwelekeo mzuri wa maendeleo. Patrick Newman na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA NEWEMAN)

Akiwa ziarani mjini Mogadishu, Bi. Clerk amekuwa na majadiliano na Rais Hassan Sheikh Mohamud, Waziri Mkuu Omar Abdirashid Ali Sharmarke, na maafisa waandamizi wa serikali, kuhusu mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu, ushirikishwaji wa wanawake kwa asilimia 30 serikalini na uzinduzi wa mpango wa kitaifa wa maendelo kwa mara ya kwanza katika  kipindi cha miaka 30.

Mkuu huyo wa UNDP pia amekutana na wawakilishi wa asasi za kiraia, na viongozi wa wizara ya wanawake , amesema amerdhishwa na mikakati ya maendeleo ya Somalia, taifa ambalo limekuwa katika vita kwa takribani miongo mitatu.

Amesema lengo la ziara yake ni kutathmini hali ya kimaendeleo nchini humo na kuongeza kwamba wabia wa maendeleo wanafanya kile wanachopaswa kufanya katika kusaidia Somalia.