Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid ataka uwajibikaji wa ukiukwaji haki za binadamu Yemen

Zeid ataka uwajibikaji wa ukiukwaji haki za binadamu Yemen

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, leo imetoa ripoti yake iliyoweka bayana ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaotendwa na pande zote katika mzozo  nchini Yemen, inayomulika zaidi athari zake katika maisha ya raia, afya na miundombinu.

Ripoti hiyo imesema kati ya mwezi Machi na Agosti mwaka huu, tzaidi ya  raia elfu tatu wameuwawa na 6,711 wamejeruhiwa kutokana na mapigano ya Yemen.  Watu milioni 7.6 kati ya hao milioni 3  ni watoto na wanawake wanaokabiliwa na utapiamlo. Mohamed Ali-Ansour ni Mkuu wa Kitengo cha Mashariki ya Kati na Afrika Kazkazini cha ofisi ya haki za binadamu na anasema…

(Sauti ya Mohamed)

Kamishna mkuu  ametoa wito wa kuunda tume ya kimataifa itakayo chunguza kwa kina ukiukwaji wa haki za binaadamu, kwani kamisheni ya kitaifa ya uchunguzi haiwezi kuingia maeneo yoyote Yemen, na hakuna ushirikiano wowote kutoka kwa pande za mzozo”

Kamishna Zeid pia amezisihi pande zote za mzozo kujadiliana na kufikia suluhu ya kudumu kwa maslahi ya watu wa Yemen.