Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matamko ya viongozi Burundi huenda yakachochea ghasia: Adama Dieng

Matamko ya viongozi Burundi huenda yakachochea ghasia: Adama Dieng

Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uzuiaji wa Mauaji yaKkimbari, Adama Dieng,  ameelezea hofu yake kuhusu kauli za uchochezi za viongozi wa umma ambazo zinaweza kuchochea ghasia, ikiwa ni pamoja na kauli ya hivi karibuni ya afisa mwandamizi wa chama tawala cha kisiasa CNDD-FDD.Flora Nducha na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA FLORA)

Dieng amesema katika taarifa iliyotolewa Agosti 16 mwaka huu na kuchapishwa kwenye tovuti ya chama hicho Pascal Nyabenda, ambaye wakati huo alikuwa ni Rais wa chama cha CNDD-FDD na Rais wa bunge la kitaifa ilikuwa inapendekeza kwamba mauaji ya kimbari ya Rwanda yalikuwa ni uzushi wa jumuiya ya kimataifa  ambao ulitumika kuondoa serikali ya kihutu iliyokuwa mdarakani wakati huo.

Dieng amesema "kauli hii ya kutowajibika inaweza kutafsiriwa kama kukana mauaji ya kimbari", na ina uwezo wa kuchochea mgogoro wa kikabila, ndani ya Burundi na nje ya mipaka yake".

Dieng ameikumbusha serikali ya Burundi wajibu wake wa kulinda watu wake, bila kujali makabila yao au itikadi zao za kisiasa na kujizuia na vitendo vyovyote vitakavyoleta mvutano.