Ban aridhishwa na ripoti kuhusu hayati dag-hammarskjold

Ban aridhishwa na ripoti kuhusu hayati dag-hammarskjold

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, anfurahia kutangazwa upya kwa ripoti yake inayoufuata kile alichokitoa mwaka wa 2015 katika jopo huru la wataaalamu liloteuliwa naye kufuatia kauli za Baraza kuu. Jopo hilo liliundwa kushughulika na habari mapya iliyotokea kuhusu kifo cha ghalfla cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hayati Dag-Hammarskjold na wale aliosafiri nao.

katika hoja nambari 70/11 baraza kuu kufuatia pendekezo la jopo huru la wataalamu limemtaka katibu mkuu kujibu maswahili kutoka kwa nchi wanachama, na kufuatia hoja hiyo Katibu Mkuu alitoa majibu yake kwa nchi wanachama kupitia ripoti yake.

Jopo hilo pia lilipendekeza kwa katibu Mkuu kuundwa kwa maktaba ya pamoja ya kuhifadhi habari zinazotokea na Ban akajibu akisema ayari ametuma ujumbe kwa watu binafsi na mashirika husika ili kusaidia kwa hoja hiyo.

Hapo awali, Barazakuu pamoja na Katibu Mkuu walishapendekeza kuundwa kwa kamati au afisa maalum kushughulika na habari zinazotokea kwa mfano yale yaliyojiri Afrika kusini. Katibu mkuu amesema alisema habari zaidi zitatoka kwenye hifadhi za nchi wanachama na akawahimza kutafuta habari husika lakini, uamuzi wa mwisho katika jambo hili ni wa Katibu Mkuu.