Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi habari wa Brazili João Miranda do Carmo

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi habari wa Brazili João Miranda do Carmo

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO), Irina Bokova, ametoa wito wa kufanyika uchunguzi dhidi ya mauaji ya mwandishi wa habari za mitandao na mhariri João Miranda do Carmo in the Brazilian state of Goiás.

Bokova ambaye amelaani vikali mauaji hayo ameutaka uongozi kuwafikisha wahusika kwenye mkono wa sheria, ili kulinda uwezo wa waandishi wa habari wa kuendelea kuchangia kuelimisha umma.

Do Carmo, ambaye alikuwa ana miliki na kuhariri tovuti ya SAD Sem Censura, alipigwa risasi na kuuawa usiku wa Julai 24 akiwa nyumbani kwake mjini Santo Antônio do Descoberto.