Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa ajira kwa vijana unaongezeka tena:ILO

Ukosefu wa ajira kwa vijana unaongezeka tena:ILO

Shirika la kazi duniani ILO linakadiria kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana kimataifa utafifikia asilimia 13.1 mwaka huu wa 2016 na kusalia katika kiwango hicho hadi mwaka 2017. John Kibego na taarifa kamili..

(TAARIFA YA KIBEGO)

Hii ni ongezeko la asilimia 12.9 ikilinganishwa na mwaka 2015. Ripoti mpya ya ILO:mtazamo wa kimataifa wa ajira na kijamii 2016 ikiwalenga hasa vijana , inaonyesha kwamba idadi ya vijana wasiokuwa na ajira itaongezeka kwa nusu milioni mwaka huu na kufikia milioni 71 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu kushuhudia ongezeko hilo.

ILO inasema cha kusikitisha zaidi ni idadi yay a vijana hasa katika nchi zinazoendelea ambao wanaishi katika hali ya umasikini ama wa wastani au wa kupindukia licha ya kuwa wanafanya kazi. Takwimu zinaonyesha kuwa vijana milioni 156 asilimia asilimia 33.7 wanao fanya kazi wako katika hali ya umasikini ama wa wastani au wa kupindukia ikilinganishwa na asilimia 26 ya watu wazima wanaofanya kazi.