Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamko la serikali kuhusu wakimbizi wasio na vibali ni mujarabu: Mbilinyi

Tamko la serikali kuhusu wakimbizi wasio na vibali ni mujarabu: Mbilinyi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi( UNHCR) nchini Burundi,  limesema, linaunga mkono tamko la serikali ya Burundi kutangaza kutowatambua wakimbizi ambao wameondoka nchini humo bila vibali.

Katika mahojiano na idhaa hii, mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini humo Abel Mbilinyi amesema hatua hiyo ni muhimu kwa usalama wa taifa na kuwataka wakimbizi kutii agizo hilo.

( SAUTI MBILINYI)

Kadhalika Mbilinyi amesema hatua ya serikali kuunda idara maalum ya kushughulikia wakimbizi wanaorejea ni muhimu katika hatua hiyo hasa kwa kuchukulia kuwa wakimbizi waliokimbia mwaka mmoja uliopita wameanza kurejea nchini Burundi.

( SAUTI MBILINYI)