Vijana ni niongozi wa leo sio kesho:Al Hendawi

24 Agosti 2016

Tukiwa bado na kundi hilo katika jamii, Vijana hawapaswi kusubiri hadi mwisho wa dunia kuwa viongozi , wanapaswa kuwa viongozi sasa.  Huo ni ujumbe wa Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu Masuala ya Vijana, Ahmad Alhendawi, wakati akihutubia vijana katika ziara yake nchini Nigeria.

Al-hendawi amesema, viongozi bora waliomtia motisha yeye mwenyewe, na wenye mfano wa kuigwa wametoka Afrika na si pengine popote na bado bara hilo linaendelea kuzalisha viongozi bora.

Amesema akizungumzia uzoefu wake, mara nyingi, kumekuwa na tabia za kupuuza vijana na kusema vijana ni kizazi cha baadaye hivyo akatoa wito.

(SAUTI AL-HENDAWI)

“Mna usawa leo na mna usawa baadaye na mtu yeyote ambaye anajaribu kuahirisha uharaka wa kukabiliana na suala hili, basi hana uelewa”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud