Naibu mwakilishi wa UNAMID azuru kambi ya wakimbizi wa ndani Darfur:

24 Agosti 2016

Naibu mwakilishi wa pamoja wa mpango wa Umoja wa mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID, Jeremiah Nyamane Kingsley Mamabolo, amezuru kambi ya wakimbizi wa ndani ya Tawilla.

Kambi hiyo iliyoko kaskazini mwa Darfur inahifadhi zaidi ya wakimbizi wa ndani 20,000 wengi wao ni wale waliokimbia kutoka Jebel Marra kufuatia mapigano mpya yam waka huu. Naibu mwakilishi huyo Mamabolo amezuru kambi hiyo kama sehemu ya maadhimisho yam waka wa kimataifa wa vijana. Anaeleza aliyoshuhudia

(SAUTI MAMABOLO)

"Kilichokuwa bayana kwa kila mmoja , taarifa walizotoa zimepongeza ushirikiano na UNAMID , lakini kikubwa zaidi ni nia yao ya kuleta amani Sudan kwa ujumla na kuwalenga hasa vijana."

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter