Skip to main content

Ban anafutilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi DRC

Ban anafutilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi DRC

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anamefuatilia kwa makini mkutano wa leo wa kamati ya maandalizi ya mjadala wa kitaifa ulioitishwa na mpatanishi wa muungano wa Afrika Edem Kodjo huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DR Congo).

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika azimio lake nambari 2277 la (2016) lilinasisitiza umuhimu wa kuaminiana, kuwa  na mazungumzo yanayojumuisha pande zote ili kuhakikisha kushirikiano kwa mazungumzo  ya kisiasa ili kuhakikisha amani, utulivu na uwazi wakati wa uchaguzi wa rais na wabunge, sambamba inavyosema katiba ya nchi hiyo Stephane Dujarric ni msemaji wa Umoja wa Mataifa,

(SAUTI YA STEPHANE DUJARRIC)

“Katibu Mkuu kwa mara nyingine ametoa wito wa kushiriki mazungumzo ya kisiasa kwa nia njema ili kumaliza mkwamo wa mchakato wa uchaguzi. Na zaidi amezitaka pande zote kujizuia na hatua zozote zitakazoongeza mvutano au kuleta ghasia.”