Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yalaani kifo cha mpinzani Gambia:

Ofisi ya haki za binadamu yalaani kifo cha mpinzani Gambia:

[caption id="attachment_292828" align="alignleft" width="300"]hapanapaleGambia

Kifo cha mmoja wa wapinzani akiwa kizuizini huko nchini Gambia kimelaaniwa na ofisi ya Kamishna mkuu wa Haki za binadamu (OHCHR).  Ebrima Solo Kurumah ni mmoja wa watu thelathini wa kikundi cha United Democratic Party (UDP) aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitatu, baada ya kushiriki kwenye maandamano ya amani kujaribu kuleta mabadiliko kwenye upigaji kura.

Maandamano mengine yalifanyika mwezi Julai kushutumu kifo cha mkurugenzi wa chama cha UDP kanda ya vijana, Solo Sandeng aliyekufa akiwa kizuizini. Cecile Pouilly ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA CECILE POUILLY)

“Habari tulizozipata ni kwamba Bwana Kurumah aliaga dunia baada ya kufikishwa hospitalini kufanyiwa upasuaji. Inasemekana hapo awali alikuwa amenyimwa matibabu zaidi ya mara moja. Tunaomba mamlaka inayohusika kuchunguza vifo hivyo vilivyofanyika kizuizini vya mabwana Sandeng na Kurumah na malalamiko ya walio vizuizini kuwa wananyimwa huduma za matibabu”.