Dunia yakumbuka kutokomezwa kwa biashara ya utumwa

23 Agosti 2016

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Biashara ya Utumwa na Ukomeshwaji wake kote duniani ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni( UNESCO) linasema siku hii inadhihirisha jitihada kubwa ziliopigwa ulimwenguni kote  kupinga vitendo vya unyanyasaji na utumwa. Patrick Newman na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Patrick)

Katika ujumbe wake wa siku hii, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO  Irina Bokova ametaja jitihada hizo kama vile mradi wa shirika hilo uitwao  “NJIA YA UTUMWA” wenye dhamira ya kusaidia na kufadhili miradi yote inayoimarisha umoja na maendeleo kwa waathirika wa utumwa kama inavyofanywa sasa huko Brazil.

(Nats…)

Mathalani kupitia video hii wahanga wa utumwa huko Brazil na vizazi vyao vya zaza wameendelea  kuwa nguzo katika uimarishwaji wa uchumi, siasa, sanaa, utamaduni na michezo.

Na kwa mantiki hiyo Bokova amesema ndio maana wametangaza muongo mmoja wa kusherehehekea vizazi kutoka Afrika kwenda ughaibuni hadi mwaka 2024.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter